IQNA

Maulamma wawili wa Kishia wa watiwa mbaroni Makka

18:09 - September 02, 2016
Habari ID: 3470543
Vikosi vya usalama Saudia vimewatia mbaroni maulamaa wawili Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika mji mtakatiffu wa Makka.

Duru zinadokeza kuwa, Siku ya Alkhamisi,askari usalama wa Saudia leo waliwakamata wanazuoni wawili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa majina ya Sheikh Muhammad Zainuddin na Sayyid Jaafar Alawi, wenyeji wa mji wa Qatif kwa visizingizio visivyo na msingi.

Askari usalama wa utawala wa Aal Saud wamekuwa wakiwatia mbaroni kiholela wanaharakati wa kisiasa na wa kidini huko Saudia.

Kabla ya hapo pia Idara ya Mahakama ya utawala wa Aal Saud ilitekeleza hukumu ya kunyongwa Sheikh Nimr Baqir al Nimr mwanazuoni mtajika wa Saudia hatua iliyokosolewa na kulalamikiwa pakubwa na duru za ndani, kieneo na kimataifa.

Maeneo ya Qatif huko mashariki mwa Saudi Arabia yamekuwa yakishuhudia maandamano na upinzani wa wananchi dhidi ya dhulma na jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud; maandamano ambayo hata hivyo yamekuwa yakikandamizwa na askari usalama wa nchi hiyo.

3527104

captcha