IQNA

Waislamu na Wakristo Palestina wagawa futari mjini Beit Lahm

23:48 - April 10, 2022
Habari ID: 3475109
TEHRAN (IQNA)- Waislamu na Wakristo wa Palestina wamekuwa wakishiriki katika mpango wa pamoja wa kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa,  mpango huo unajumuisha kupamba soko na mitaa sambamba na kugawa tenda na maji wakati wa futari katika miji kama vile Beit Lahm (Bethlehemu), Ramallah, na Nablus katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Khalil Kawa, 41, ni Mkristo ambaye amekuwa akigawa tende na maji ya kunywa kwa wapiti njia mjini Nablus. Huu ni mji wa Kipalestina ambao una Waislamu, Wakristo na Wasamaria ambao wanaishi pamoja kwa amani.

“Sihisi kama ni jambo lisilo la kawaida kwa Mkristo kugawa tenda na maji kwa Waislamu wanaofunga Saumu ya Ramadhani. Sipende kutofautisha baina ya Muislamu, Mkristo au Msamaria kwani sote ni Wapalestina.” Anasema hata wakati wa Mulid ya Mtume Muhammad SAW, wao huzunguza katika mji wa Nablus kugawa peremende na katika Mwezi wa Ramadhani hugawa tende na maji kwa waumini.

Kawa anasema awali alikuwa akifadhili mradi huo lakini sasa kuna marafiki zake wengi waliojiunga naye na hivyo huwa na fedha za kutosha za kugharamia mradio huo.

3478434

Kishikizo: palestina beit lahm
captcha