IQNA

Viwango vitatu vya Saumu ya Ramadhani

18:27 - April 11, 2022
Habari ID: 3475115
TEHRAN (IQNA)- Katika Saumu ya Ramadhani, waumini hawali au kunywa lakini ni wazi kwamba kufunga sio tu kuweka kujizuia kunywa na kula.

Ili mwenye kufunga Saumu ya Ramadhani aweze kutakasika kwa maana halisi ya neno na kuepuka dhambi yoyote katika mwezi huu mtukufu basi ni lazima azingatie pia tabia na mienendo yake binafsi.

Kufunga saumu ya Ramadhani ni faradhi ya kidini ambapo Mwislamu hujizuwia kula na kunywa katika baadhi ya siku kuanzia kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwa jua. Mtu huyu anaitwa mfungaji na hali hii hii inaitwa kufunga.

Lakini katika mafundishi ya Kiislamu, saumu ni zaidi kutokula au kunywa, na inasisitizwa kwamba mfungaji anahitaji kujitunza zaidi.

Ayatollah Mojtahed Tehrani (1923-2013), mmoja wa wanazuoni  wa ngazi za juu wa akhlaqi, maadili na falsafa nchini Iran, anaamini kuwa funga ina viwango vitatu. Saumu ya kwanza ya jumla;  ya pili ni maalum nay a tatu ni maalum zaidi.

Ngazi ya kwanza inahusiana na funga ambayo mfungaji anajaribu kujizuia kula na kunywa. Hiki ndicho kiwango cha funga ambacho Waislamu wote wanalazimika kukizingatia; Hiyo ina maana kuwa, wanajaribu kutokula au kunywa chochote, lakini hawatunzi sehemu zingine za mwili wao.

Ngazi ya pili na maalum ya kufunga ina maana kuwa,  mfungaji pamoja na kuacha kula na kunywa, pia hufunga sehemu zote za mwili wake. Macho yake, masikio yake, ulimi wake, mikono yake na miguu yake, na viungo vyote vya mwili wake vinajiepusha na dhambi. Anajaribu kufumba macho yake ili kujizuia kutenda dhambi; Yeye huziba masikio yake yasiweze kusikia maneno ya dhambi; Hasemi maneno machafu na wala hafanyi dhambi kwa mikono na miguu yake.

Lakini ngazi ya tatu ya kufunga ni maalum zaidi; Saumu ambayo inahusishwa na kumkumbuka Mwenyezi Mungu na mfungaji hafanyi kitu kingine isipokuwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu moyoni mwake. Mfungaji katika kiwango hiki, katika maombi yake, machozi hutoka machoni mwao kwa furaha na hofu ya Mwenyezi Mungu; Maombi yake ni ya kimapenzi na huwa na hamu kubwa sana wakati wa kuomba na kuwasiliana na Mwenyezi Mungu.

3893571

captcha