IQNA

Dhifa ya futari ya umma yaruhusiwa tena Qatif, Saudi Arabia

17:47 - April 26, 2022
Habari ID: 3475172
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa madhehebu ya Shia katika kijiji cha Umm al Himam katika eneo la Qatifa nchini Saudia Arabia Jumatatu walishiriki katika dhifa ya futari ya umma kwa mara ya kwanza tokea lianze janga la corona.

Vijana wa kijiji hicho waliandaa dhifa hiyo ya futari ambayo iliwaleta pamoja waumini zaidi ya 200. Aidha barabara za kijiji hicho zilipambwa kwa mata na bendera na kuibua mandhari yenye mvuto, amesema Tayseer Muhammad mmoja kati ya walioandaa dhifa hiyo.

Amesema wakazi walikuwa na furaha kushiriki na kukutana katika kikao hicho cha pamoja cha futari hii ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mjumuiko kama huo katika kipindi cha miaka miwili.

Mnamo Machi 22, Saudi Arabia ilitangaza kurudisha itikafu katika misikiti miwili mitakatibu ya Makka na Madina (Masjid al-Haram na Masjid al-Nabi) wakati wa Ramadhani mwaka huu, baada ya kusitishwa kwa  miaka miwili kuanzia Machi 2020 ili kuzuia maambukizi ya coron.

Kwa upande mwingine mijumuiko ya futari imeruhusiwa tena katika nchi hii, na Wizara ya Miongozo na Masuala ya Kiislamu ya Saudia ilitoa amri kuhusiana na hili.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi pia imeondoa kanuni zilizokuwa zinatakelezwa za kuzuia kuenea corona zikiwemo za kutokaribiana waumini  Msikiti Mkuu wa Makkah, Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina na misikiti mingine. Aidha si sharti tena waumini kuvaa barakoa.

 

captcha