IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari Yunes Shahmoradi wa Iran Ameshinda Shindano la Qur'ani la Otr Elkalam la Saudi Arabia

11:51 - April 08, 2023
Habari ID: 3476831
TEHRAN (IQNA) – Yunes Shahmoradi kutoka Iran ameibuka mshindi katika toleo la pili la Shindano la Kimataifa la Qur’ani Tukufu la Otr Elkalam nchini Saudi Arabia.

Alikuwa miongoni mwa wasomaji wanne wa Qur'ani waliokuwa wamefika kwenye fainali ya shindano hilo la Qur'ani Tukufu.

Shahmoradi alipokea zawadi ya fedha taslimu riyal milioni tatu za Saudia au USD 800,000 kwa kuchukua nafasi ya kwanza katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani.

Wengine watatu walioingia fainali katika kitengo hiki walikuwa Abdul Aziz Faqih kutoka nchi mwenyeji aliyemaliza mshindi wa pili na Wamorocco Zakariya al-Zirak na Abdullah Al-Dughri waliibuka wa tatu na wa nne mtawalia.

Katika kategoria ya Adhana, washindani kutoka Saudi Arabia, Indonesia, Lebanon na Uingereza walishinda nafasi nne bora, mtawalia.

Toleo la pili la shindano la kimataifa la Qur'ani la Otr Elkalam liliandaliwa  Mamlaka ya Burudani ya Jumla Saudia (GEA).

Shindano hilo liliianza siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani (Machi 23).

Waandalizi wanasema moja ya malengo yao yalikuwa ni kuangazia wingi wa tamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu, kupitia kusoma Qur'ani Tukufu na Adhana..

Mwaka huu, shindano hilo lilivutia washiriki 50,000 Waislamu kutoka zaidi ya nchi 100, wote wakiwania kufuzu.

Kati ya washiriki 2,116 walioshinda, washiriki 36 (18 katika qiraa au usomaji Qur'ani na 18 katika adhana) walifuzu kwa hatua za mwisho.

Jumla ya pesa za tuzo za shindano hilo zilizidi riyal milioni 12 za Saudi ($ 3.2 milioni).

4132133

captcha