IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Makka yanaanza leo

16:18 - August 25, 2023
Habari ID: 3477495
MAKKA (IQNA)- Toleo la 43 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Saudi Arabia litaanza leo katika mji mtakatifu wa Makka huku wawakilishi kutoka nchi 117 wakishiriki.

Mji mtakatifu wa Makaa unaandaa toleo la 43 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Mfalme Abdulaziz  katika kuhifadhi, kusoma na kutafsiri.
Mashindano hayo yanayoanza leo yatafanyika kwa siku 11 kwenye Msikiti Mkuu wa Makka (Al Masjid Al Haram) eneo takatifu zaidi katika Uislamu.
Hafla hiyo imeandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, na kupewa jina la mwanzilishi wa marehemu wa Saudi Arabia, Mfalme Abdulaziz.
Mashindano ya mwaka huu yamevutia washiriki 166 kutoka nchi 117, kwa mujibu wa msimamizi mkuu wa wizara hiyo Abdelatif Al Alsheikh.
Aliongeza kuwa jumla ya thamani ya zawadi hizo imeongezeka na kufikia zaidi ya dola milioni moja mwaka huu, huku mshindi bora akipata dola 133,000. Wizara imekuwa ikifanya mashindano hayo ya kila mwaka tangu 1979.

3484916

captcha