IQNA

Waislamu Ufaransa

Waislamu wa Ufaransa wanahitaji kanuni mpya za kuendesha shughuli zao

21:06 - September 18, 2023
Habari ID: 3477620
PARIS (IQNA) - Edouard Philippe, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu chini ya Rais wa Ufaransa Emanuel Macron kutoka 2017-2020, almeandika katika kitabu chake kipya kilichotolewa Des Lieux Qui Disent (Maeneo Yanayozungumza) kwamba kuna haja ya kuunda "kanuni na shirika maalum kwa ajili ya kusimamia masuala ya Waislamu”.

Katika mahojiano juu ya Inter, Philippe alielezea zaidi maoni yake, akisema sheria ya Ufaransa ya 1905, ambayo inasisitiza kutofuata dini, "labda haina uwezo wa kushughulikia mambo maalum ya Uislamu."

Alisema kwamba kupendekeza aina fulani ya makubaliano, ambayo ni taratibu maalum ya kusimamia masuala ya Waislamu ndani ya jamii ya Wafaransa, inapaswa kuwa mezani.

Imesemekana kwa muda mrefu kwamba msisitizo uliokithiri wa Ufaransa juu ya kutokuwa na dini tayari unalenga vibaya Uislamu ambapo serikali ya nchi hiyo inatuhumiwa kuwachukulia Waislamu kama raia wa kikoloni ambao ni wageni kwa Ufaransa badala ya raia waliojumuishwa kikamilifu.

Marufuku ya abaya, vazi la kujisitiri linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu, iliyoanzishwa katika shule za Ufaransa mwezi huu imetajwa kuwa mfano mmoja wa hivi karibuni.

Serikali ya Ufaransa, inayoongozwa na Macron, imeshutumiwa kwa chuki dhidi ya Uislamu na mateso dhidi ya Waislamu kwa kisingizio cha kutokuwa na dini na kupinga ugaidi. Darmanin alisaidia kupitisha sheria ya 2021 ya "kupinga utengano", ambayo wanaharakati wanasema inalenga Waislamu na inaharamisha Uislamu katika mashirika ya kiraia. Mtazamo wa serikali ya Ufaransa umekosolewa kwa kukosa kuchochea misimamo mikali huku ikidai kupambana nayo.

3485208

Kishikizo: ufaransa waislamu
captcha