IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 46 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran Yaanza

20:22 - December 01, 2023
Habari ID: 3477970
TEHRAN (IQNA) - Duru ya mwisho ya toleo la 46 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran ilianza katika mji wa kaskazini-magharibi wa Bojnourd siku ya Ijumaa asubuhi.

Sherehe ya uzinduzi wa hafla hiyo ilifanyika Alhamisi usiku na viongozi, washindani, na kundi kubwa la watazamaji walihudhuria.

Sherehe ilianza kwa usomaji wa aya za Surah Ghafir na qari wa kimataifa wa Iran Hadi Esfidani.

Maafisa kadhaa walihutubia tukio hilo, wakiangazia nafasi ambayo Qur'ani Tukufu katika kuwaongoza wanadamu katika nyanja tofauti za maisha.

Hadhirina pia waliwakumbuka na kuwaombea Dua maelfu ya Wapalestina ambao wameuawa katika Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Israel tangu tarehe 7 Oktoba huku pia wakikashifu vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Washindani wanaume na wanawake watashindana katika kategoria tofauti kama vile usomaji na kuhifadhi Qur'ani, Tarteel, usomaji wa Adhana, na Qasida.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Shirika la Wakfu na Hisani la Iran yataendelea hadi Desemba 9

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kila mwaka kwa kushirikisha makari na wahifadhi wa Qur'ani wakuu kutoka kote nchini.

Mashindano hayo hulenga kugundua vipaji vya Qur'ani Tukufu na kustawisha shughuli za Qur'ani katika jamii.

Washindi wakuu wa mashindano hayo wataiwakilisha Iran katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur'ani kote duniani.

3486237

Habari zinazohusiana
captcha