IQNA

Nchi 50 kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya wanachuo

23:02 - July 29, 2016
Habari ID: 3470481
Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu yatakayofanyika Iran yanatazamiwa kuwa na washiriki kutoka nchi Zaidi ya 50.

Hamid Saber Farzam ameliambia Shirika la Habari la IQNA kuwa, mashindano hayo yamepangwa kufanyika mapema Januari (1-4) mwaka 2017 katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran. Ameongeza kuwa, mbali na kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu, mashindano hayo yatakuwa pia kwa mara ya kwanza yatakuwa na kategoria ya utafiti wa Qur’ani Tukufu.

Aidha amesema wawakilishi wa kila nchi, wakiwemo Wairani, watashiriki katika mashindano baada ya kufanyiwa mtihani na wataalamu wa Qur’ani wa kamati andalizi.

Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanachuo Waislamu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

3518131

captcha