IQNA

Nusu Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi yakamilika

12:00 - March 27, 2018
Habari ID: 3471445
TEHRAN (IQNA)- Nusu Fainali ya Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu imemalizika.

Hayo yamedokezwa na Bw. Hamid Saber Farzam Mkuu wa Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran iliyoandaa mashindano hayo ambayo fainali zake zitafanyika Aprili 27.

Amesema hadi kufika kiwango cha semi fainali, mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kwa njia ya simu au kutuma faili za sauti kutoka maeneo mbali mbali duniani. Katika awamu za kwanza wanafunzi 203 kutoka vyo vikuu vya nchi 73 duniani walishiriki kwa kutuma faili za sauti ambapo 100 kati yao walifika semi fainali. Mashindano ya semi fainali yalifanyika kwa njia ya simu ambapo hatimaye wanafunzi 40 walifika fainali ambayo itafanyika kwa muda wa siku tatu katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.

Ameongeza kuwa katika siku ya mwisho la fainali, washiriki watakutana na Kiongozi Muadhamuwa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran inayofungamana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

3701767

captcha