IQNA

Jinai za Israel

Palestina yataka IAEA ichukue hatua dhidi ya Israel baada ya kutishia kudondosha bomu la nyuklia Gaza

13:46 - November 10, 2023
Habari ID: 3477870
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amewasilisha faili mbele ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kulalamikia matamshi ya vitisho ya waziri wa utawala wa Kizayuni kwamba ikilazimu, utawala huo haramu utatumia bomu la nyuklia dhidi ya watu wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la WAFA, Riyad al-Maliki amemtumia barua Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA akilaani vitisho hivyo na kusisitiza kuwa: Tishio hilo la kutumia bomu la nyuklia linaenda sambamba na mwenendo uliochukuliwa na Israel hivi sasa dhidi ya Wapalestina.

Al-Maliki ameongeza kuwa, tishio la afisa huyo wa serikali ya Tel Aviv linathibitisha kwamba, utawala huo pandikizi unamiliki silaha za nyuklia na za maangamizi ya umati. Israel inakadiriwa kuwa na vichwa vya nyuklia 200 hadi 400 katika ghala lake la silaha, na kuifanya kuwa mmiliki pekee wa silaha zisizo za kawaida Magharibi mwa Asia au Mashariki ya Kati

Siku chache zilizopita, Amihai Eliyahu, Waziri wa Turathi wa utawala wa Kizayuni katika baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu alitoa wito wa kulipuliwa Gaza kwa bomu la nyuklia.

Mwanasiasa huyo alikiri kuhusu mauaji ya umati yanayotekelezwa na utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya watu wa Gaza na kusema kuwa, kutumika bomu la nyuklia ni njia mojawapo za kutoa kipigo kikali zaidi dhidi ya Gaza.

Makundi ya muqawama yamesema matamshi ya waziri huyo wa utawala ghasibu wa Israel kuhusu uwezekano wa kudondoshwa bomu la nyuklia huko Gaza yanaonyesha ugaidi wa utawala huo dhidi ya taifa la Palestina.

Aidha Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema kwamba, “Kwa mara nyingine tena, afisa wa utawala wa Kizayuni amekiri kumiliki silaha za nyuklia. Muhimu zaidi, alidharau kanuni za kimsingi za sheria ya kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kutoa vitisho dhidi ya watu wanaodhulumiwa na wasio na hatia wa Gaza."

3485941

Habari zinazohusiana
captcha