IQNA

OIC yalaani hatua ya Israel kubomoa nyumba za Wapalestina

15:54 - November 10, 2020
Habari ID: 3473346
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa taarifa ikilaani uhalifu unaoendelea kufanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel wa kubomoa nyumba na taasisi za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imesisitiza kuwa operesheni ya kuharibu nyumba na taasisi za Wapalestina na kulazimisha makumi ya familia zao kuishi ukimbizini vinafanyika katika fremu ya mipango ya utawala haramu wa Israel.

OIC imesema kuwa hatua hiyo inakiuka sheria za kimataifa na maazimio la Baraza la Usalama. Vilevile imeitaja jamii ya kimataifa kuzidisha mashinikizo dhidi ya utawala huo ili ukomeshe uhalifu huo. 

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umelaani na kukemea zoezi la utawala ghasibu wa Israel la kuharibu nyumba za raia wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. 

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mwaka huu wa 2020 utawala wa Kizayuni wa Israel umebomoa nyumba karibu 689 katika Ukingo wa Magharibi na Quds tukufu na kuwalazimisha Wapalestina 869 kuwa wakimbizi.  

3934404

captcha