IQNA

Spika wa Bunge la Iran yuko Uturuki kushiriki mkutano wa mabunge ya Kiislamu

21:28 - December 08, 2021
Habari ID: 3474656
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) yuko nchini Uturuki kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Mabunge ya Kiislamu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC)

Kwa mujibu wa taarifa, Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf aliwasili Uturuki  Jumatano na kulakiwa na Osman Nuri Gülaçar,Mwenyekiti wa Kundi la Kirafiki la Mabunge ya Iran na Uturuki.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Nuri amesisitiza kuhusu nafasi muhimu ya Iran katika eneo na kusema: "Inatazamiwa kuwa nchi hizi mbili zitachukua hatua za kuboresha uhusiano zaidi hadi ifikapo mwaka 2023."

Aidha amesema mabunge ya nchi hizi mbili yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha uhusiano.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Iran ameashiria uhusiano wa mabunge ya Iran na Uturuki na kusema uhusiano wa nchi mbili uko katika kiwango kizuri na cha kurihdhisha na inatazamiwa kuwa uhusiano huo tazidi kuboreka.

Mkutano wa 16 wa  Jumuiya ya Mabunge ya Kiislamu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu unafanyika Istanbul Uturuki kuanzia Disemba 9-10 na mada kuu ni "Palestina, Uhamiaji na AfghanIstan.

84570502

captcha