IQNA

UN yalaani mashambulizi dhidi ya mwanahabari Muislamu India

23:16 - February 23, 2022
Habari ID: 3474966
TEHRAN (IQNA)- Wataalamu wa haki za Umoja wa Mataifa wametaka kukomeshwa kwa mashambulizi ya mtandaoni "ya kuchukiza dhidi ya wanawake na ya kimadhehebu" dhidi ya mwanahabari Muislamu nchini India, wakiomba mamlaka kuchunguza unyanyasaji huo.

Rana Ayyub, mkosoaji mkali wa Waziri Mkuu Narendra Modi na itikadi ya utaifa wa Kihindu katika chama chake cha Bh aratiya Janata (BJP), amekuwa mlengwa wa kampeni isiyokoma ya unyanyasaji mtandaoni - ikiwa ni pamoja na vitisho vya kifo na ubakaji.

Yeye ndiye "mwathirika wa mashambulizi na vitisho vinavyoongezeka mtandaoni kutoka kwa vikundi vya siasa za mrengo wa kulia za Kihindu", wanahabari huru, ambao hawazungumzi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa lakini wamepewa jukumu la kuripoti kwa umoja huo, walisema katika taarifa Jumatatu (Feb 21).

Walisema mashambulio haya yalitokana na kuripoti kwa Ayyub juu ya maswala yanayoathiri Waislamu walio wachache wa India, ukosoaji wake wa jinsi serikali inavyoshughulikia janga la Covid-19, na maoni yake juu ya marufuku ya hivi karibuni ya hijabu katika shule na vyuo katika jimbo la kusini la Karnataka.

Waandishi hao wameongeza kuwa serikali ya India imeshindwa kulaani au kuchunguza mashambulizi hayo.

"Amekuwa akinyanyaswa kisheria na mamlaka ya India kuhusiana na kuripoti kwake", walisema, ikiwa ni pamoja na kufungiwa kwa akaunti yake ya benki na mali nyingine.

Ayyub, 37, alianza kama mwandishi wa habari za uchunguzi na aliandika kitabu akimshutumu Waziri Mkuu Narendra Modi kwa kushiriki katika ghasia mbaya za kidini huko Gujarat mnamo 2002, alipokuwa waziri mkuu wa serikali ya jimbo

Tangu wakati huo amekuwa mtoa maoni wa magazeti ya kimataifa vyombo vingine vya habari.

Waandishi wengine wa habari pia wamelalamikia kuongezeka kwa unyanyasaji chini ya Modi, ambaye serikali yake inashutumiwa kwa kujaribu kunyamazisha ripoti muhimu.

Kundi la haki za vyombo vya habari lijulikanalo kama Reporters Without Borders (RSF) linaiweka India katika kiwango cha chini cha 142 katika Fahirisi yake ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ikisema kwamba chini ya Modi, "shinikizo limeongezeka kwa vyombo vya habari ambavyo vinalazimishwa kufuata mstari wa serikali yenye misimamo ya kitaifa ya Kihindu".

"Kampeni zilizoratibiwa za chuki zinazoendeshwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya waandishi wa habari wanaothubutu kuzungumza au kuandika kuhusu mada ambazo zinawaudhi wafuasi wa Hindutva (itikadi kali ya Kihindu) ni za kutisha na zinajumuisha wito wa kuwataka wanahabari wanaohusika kuuawa," kulingana na RSF.

"Kampeni zina vurugu hasa wakati walengwa ni wanawake."

3477927

captcha