IQNA

Hali ya Waislamu India

Taasisi ya Haki za Binadamu OIC yalaani ubaguzi, ukiukaji wa haki za Waislamu wa India

17:33 - June 21, 2022
Habari ID: 3475404
TEHRAN (IQNA) - Taasisi ya haki za binadamu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu nchini India.

Taasisi hiyo imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuiwajibisha India kwa ukiukaji wa haki za binadamu za walio wachache na kukomesha uhasama wao.

Tume Huru ya Kudumu ya Haki za Kibinadamu (IPHRC), mojawapo ya vyombo vikuu vya OIC yenye wanachama 57, iliandika kwenye Twitter kwamba inalaani "vitendo hivi  vya kikatili vya ubaguzi, vinavyokiuka maadili yote ya jamii anuai na ambavyo vinafanyika kwa kupuuza sharia kabisa!!

IPHRC imetoa wito kwa jamii ya kimataifa na hasa taasisi husika za Umoja wa Mataifa kuitaka serikali ya India kulinda haki za binadamu za Waislamu waliowachache nchini humo na kusitisha mara moja uhasama dhidi yao. Aidha asasi hiyo ya OIC imezitaka taasisi  Umoja wa Mataifa kuhimiza serikali ya India haki za binadamu za  Waislamu walio wachache na kukomesha mara moja uhasama dhidi yao.

Tume hiyo pia imesembaza klipu ya Arundhati Roy, mwanaharakati na mwandishi maarufu wa India, akielezea jinsi India ilivyogeuka na kuwa "biashara ya kifashisti ya Kihindu (Kibaniani)."

Roy amesema, "Ubomoaji wa nyumba za Waislamu unaashiria wakati fulani ambapo unaona mabadiliko kutoka kwa aina ya demokrasia dhaifu na yenye dosari inayobadilika kwa uwazi, na kwa ujuba kuwa biashara ya kifashisti ya Kihindu itendayo jinai."

Mwanaharakati huyo amesema dalili zote zinaonyesha jinai hizo zinaungwa mkono katika ngazi zote za serikali kuanzia "mamlaka ya manispaa, mahakimu wa mitaa, vyombo vya habari na juu ya yote mahakama ambazo zinaangalia pembeni na hazifanyi chochote."

Amesema kwa kuzingatia nukta hizo , kinachofanyika  ni kuwaambia Waislamu wakopeke yao na hawatapata msaada wowote na wala sharia za India hazitawatetea. Kwa hivyo taasisi zote ambazo zilikuwa sehemu ya udhibiti na mizani ya demokrasia ya zamani  nchini humo sasa zitatumika kama silaha dhidi ya Waislamu.

Watawala katika majimbo yanayotawaliwa na chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi, Bharatiya Janata Party (BJP), katika miezi ya hivi karibuni wameanza kubomoa nyumba, maduka na biashara ambazo ni za Waislamu, kwa tuhuma za kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali.

Wiki iliyopita, baada ya kutuma mabuldoza huko Kanpur na Saharanpur, utawala wa Uttar Pradesh ulibomoa nyumba ya mwanaharakati wa wanafunzi Afreen Fatima huko Prayagraj baada ya kutoa notisi ya siku moja tu ya kuondoka, kufuatia maandamano dhidi ya matamshi ya dharau kuhusu Mtume Muhammad (SAW) yaliyotoelwa na wasemaji wa BJP.

Kauli ya IPHRC kuhusu dhuluma dhidi ya Waislamu nchini India inakuja baada ya tume hiyo kuidhinisha lawama na hasira zilizoonyeshwa na OIC na wanachama wa jamii ya kimataifa kutokana na matamshi machafu yaliyotolewa na viongozi wa BJP dhidi ya Mtume Mtukufu Muhammad (SAW).

Mnamo Juni 6, IPHRC ilituma ujumbe katika Twitter na kuandika: "OIC-IPHRC inautaka Umoja wa Mataifa na asasi za haki za binadamu duniani kuishinikiza India kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na matamshi ya matusi, kuwashtaki wale wanaohusika bila mapendeleo na kusitisha mateso yake ya kimfumo dhidi ya Waislamu walio wachache."

3479397

Kishikizo: india waislamu oic bjp modi
captcha