IQNA

Ibada

Sala ya Istisqa kusaliwa katika Haram ya Imam Ridha (AS)

16:50 - January 18, 2024
Habari ID: 3478211
IQNA – Sala ya Istisqa (ya kuomba mvua) imepangwa kusaliwa kwenye haram tukufu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

Sala hiyo inaswaliwa leo Alhamisi, Januari 18, baada ya Sala ya Maghrib na Isha katika eneo la Sheikh Tousi Bast la haram hiyo takatifu.

Watu wa Mashhad na waumini wanaozuru eneo hilo takatifu wanatarajiwa kushiriki katika ibada hiyo.

Soma zaidi

Sala ya Istisqa (ya kuomba mvua) kusaliwa kote UAE

Istisqa maana yake ni kumuomba Mwenyezi Mungu ateremshe mvua wakati wa ukame na nyakati za mvua chache. Haya yalifanywa na Mtume Muhammad (SAW). Kwa mujibu wa riwaya Mtume Muhammad (SAW) alikwenda kwenye uwanja wa kusali kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu ateremshe mvua ya neema. Inaelezwa kuwa alielekea Qiblah, huku akiwa amevua joho lake ambapo aliswali rakaa mbili.

Salatul-Istisqa inajuzu kunapokuwa na ukame na mvua chache, au kiwango cha maji katika mito na 

captcha